Rais Magufuli afanya uteuzi wa Kamishna mpya wa Magereza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza Phaustine Martin Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza kuanzia leo Julai 13.

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike amechukua nafasi ya aliyekuwa Kamishna wa Magereza Dkt. Juma Alli Malewa ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huu Kamishna Jenerali wa Magereza Kasike alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga, DSM.

Kamishna wa Magereza atimuliwa kikaoni na Waziri Lugola Kisa ? (+Video)

Julai 6 mwaka huu 2018, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemfukuza kwenye kikao Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW