Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti wa chuo cha ATC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha – ATC.

Prof. Tumbo ni Mkuu wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC).

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Musa Iyombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW