Habari

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Naibu Waziri na Katibu Mkuu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Dkt. Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma anachukua nafasi ya Dkt. Susan Alphonce Kolimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents