Tupo Nawe

Rais Magufuli afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, Amteua Kichere kuwa CAG mpya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli leo Novemba 3, 2019 amemteua Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Kichere anachukua nafasi ya Prof. Mussa Assad ambaye kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano kinaishia kesho Novemba 4, 2019.

Mteule huyo, Alishawahi kuwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), N alitenguliwa uteuzi wake na Rais Magufuli na kisha kumteua tena kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Juni 8, mwaka huu.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amewateua Aisha Amour kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Kanali Francis Mbindi kuwa kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu na majaji 12 wa Mahakama Kuu, Viongozi wote wataapishwa kesho Novemba 4, 2019.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW