Habari

Rais Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti 7 wa bodi ya taasisi za serikali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli afanya uteuzi wa wenyeviti 7 wa baadhi ya bodi ya taasisi za serikali.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 19 Desemba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja walioteuliwa kama ifuatavyo:

Rais Magufuli amemteua Bw. Ali Mufuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira.

Bw. Ali Mufuruki ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni za Infotech Investment na Mwenyekiti wa Taasisi ya Afrika inayojihusisha na uendelezaji wa vipaji vya uongozi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais Magufuli amemteua Mhandisi Christopher Kajolo Chiza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)

Mhandisi Christopher Kajolo Chiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Sabetha Mwambenja ambaye amemaliza muda wake.

Rais Magufuli amemteua Bw. Peter M. Maduki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
Bw. Peter M. Maduki anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Idrissa Mshoro ambaye amemaliza muda wake.

Rais Magufuli amemteua Dkt. Yamungu Kayandabila kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).
Dkt. Yamungu Kayandabila ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Peter Ilomo ambaye amemaliza muda wake.

Rais Magufuli amemteua Prof. Godwin Daniel Mjema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Huduma za Fedha na Mikopo (UTT-MFI)
Prof. Godwin Daniel Mjema ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Fadhili D. Mbaga ambaye amemaliza muda wake.

Rais Magufuli amemteua Kepteni Ernest Mihayo Bupamba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Chuo cha Bahari (DMI)
Kepteni Ernest Mihayo Bupamba ni Mwendesha Meli Mkuu (Principal Captain) Katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce S. Hepelwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Miradi ya Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID)
Dkt. Aloyce S. Hepewa ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. John Jingu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Tanzania.
Dkt. John Jingu ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Dkt. Rashid Adam Tamatama kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI).
Dkt. Rashid Adam Tamatama ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pia, Rais Magufuli amemteua Bibi. Zuhura Muro kuwa Mjumbe wa Baraza la Taifa la Biashara (Tanzania National Business Council – TNBC).
Bibi. Zuhura Muro ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi inayojihusisha na huduma za ushauri wa ubora na mafunzo (Service Limited) katika ofisi zake za Dar es Salaam.

Wateule wote waliotajwa hapo juu, uteuzi wao umeanza tarehe 17 Desemba, 2016

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents