Aisee DSTV!

Rais Magufuli ahani msiba wa Abbas Tarimba na kutoa pole kwa Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Dkt. Sadala aliyefiwa na mkewe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumapili Juni 23, 2019 ametoa mkono wa pole kwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Abdallah Sadala “Mabodi” ambaye amefiwa na mkewe Dkt. Badria Abubaker Gunar aliyefariki dunia jana jijini Dar es salaam.

Baadaye Mhe. Rais Magufuli alienda kuhani msiba kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni ya SportPesa, Bwana Abbas Tarimba Abbas, ambaye hivi karibuni amefiwa na watoto wake wawili.  Mmoja alifariki dunia miezi mitatu iliyopita na mwngine wiki iliyopita jijini Dar es salaam.

Baada ya matukio hayo mawili, Rais Magufuli aliungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es salaam, kusali Misa Takatifu ya Sherehe ya Ekaristi Takatifu kanisani hapo.

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW