Habari

Rais Magufuli airudia kauli yake kwa Mpoto ‘sichoki kusikiliza nyimbo zako’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Jumatano hii amefungua mradi wa nyumba 150 za mradi wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu, kata ya Iyumbu Mkoani Dodoma.

Rais John Pombe Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali wakipata picha ya pamoja na bendi ya Mrisho Mpoto

Katika uzinduzi huo msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto akiwa pamoja bendi yake, Mpoto Band alitoa burudani ya aina yake na kuwavutia viongozi wa serikali waliojitokeza katika uzinduzi huo.

Mrisho Mpoto na bendi yake wakitoa burudani katika uzinduzi huo.

Baada ya uzinduzi huo kumalizika, muimbaji huyo aliitwa na Rais John Pombe Magufuli kwaajili ya picha ya pamoja ambapo pia akipata fursa ya kuzungumza na rais mambo kadhaa kuhusu muziki wake.

Akiongea na mwandishi wetu muda mchache baada ya picha hizo, Mpoto alisema bado rais anairudia kauli yake ya kusema kwamba anaupenda sana muziki wake na achoki kuusikiliza.

“Ni kweli niliitwa nikapiga naye picha baada ya hapo akawa anasema anaupenda sana muziki wangu, anaisikiliza sana Sizonje,” alisema Mpoto.

Aliongeza, “Mimi binafsi hiyo kauli yake sio mara ya kwanza kuisema, amekuwa akiirudia mara kwa mara na imenifanya nifikirie vitu ngingi sana, unajua kuandaa wimbo ambao utamfanya rais wa nchi kila akikaa auzungumzie ni kitu kikubwa sana na jambo ambalo linanifanya nione nimefanya kazi kubwa sana na pia namshukuru kwa kuendelea kuusikiliza muziki wangu kwa sababu kama unavyojua wasanii ni wengi sana, rais akipata fursa ya kuzikiliza nyimbo yako kila mara ni jambo la heri sana,”

Angalia picha za uzinduzi wa mradi huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefungua mradi wa Nyumba za Gharama nafuu Iyumbu Satellite Centre Jumatano hii. Mradi huo una jumla ya nyumba 150 kwa awamu ya kwanza na zitafuata nyumba zingine 150 katika awamu inayofuata .


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu, na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk.Benilith Mahenge wakimkaribisha Mheshimiwa Rais Dk John Pombe Magufuli


Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya NHC, Mama Blandina Nyoni.

Meneja wa Miradi ya Ubia, Subira Gudadi akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson wakati akiwasili katia eneo la mradi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents