Habari

Rais Magufuli akwara tuzo ya heshima ya ukuzaji kiswahili Afrika

Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili wa Vyuo Vikuu vya Tanzania (CHAWAKITA) kimetoa Tuzo ya Heshima kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli kutokana na mchango wake mkubwa wa kuthamini na kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania.

Image result for rais magufuli tuzo
Rais Magufuli

Tuzo hiyo, imetolewa na chama hicho na kupokewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Juliana Shonza kwa niaba ya Rais Magufuli.

Alipokea tuzo hiyo juzi mjini Morogoro wakati akifunga kongamano la 11 la kitaifa la Chawakita lililofanyika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.

Kongamano hilo la siku nne lilibeba kaulimbiu inayosema, “Kiswahili, Hazina ya Afrika kwa Maendeleo Endelevu” na kuandaliwa kwa tuzo kwa washindi wa uandishi wa vitabu vya hadithi fupi pamoja na ya heshima ambayo aliyotunukiwa Rais Magufuli kutokana na anavyoenzi na kukitilia maanani Kiswahili.

Pia tuzo nyingine ya heshima ilitolewa kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutokana na mchango mkubwa wa wizara hiyo katika kusimamia na kuendeleza lugha ya Kiswahili nchini.

Chanzo: https://habarileo.co.tz/habari/2019-03-265c99b7900dbdb.aspx

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents