Habari

Rais Magufuli alitaka Jeshi la Magereza kutumia wafungwa kwa uzalishaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John P. Magufuli leo ametia saini nyaraka za msamaha kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ambapo ametumia fursa hiyo pia kulitaka jeshi la Magereza kuwatumia wafungwa kwa uzalishaji.

Rais Dkt. John Magufuli akitia saini nyaraka za msamaha alioutoa kwa wafungwa 61 waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa na wawili Nguza Viking (Babu Seya) na Johnson Nguza (Papii Kocha) waliohukumiwa kifungo cha maisha jela.

Rais Magufuli ametia saini nyaraka hizo leo Jumapili Desemba 10,2017 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, ikiwa ni siku moja tangu atangaze msamaha kwa wafungwa 8,150.


Kwa upande mwingine Rais Magufuli amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri ya kurekebisha tabia za wafungwa huku akilitaka jeshi hilo kuhakikisha linawatumia wafungwa kuzalisha mali, yakiwemo mazao ya kilimo na kufanya kazi za ujenzi.

Nimeona nitumie kifungu hiki cha Katiba -Ibara ya 45 (1) ambacho nilipewa na Watanzania, ingawa kilikuwa hakijawahi kutumika, unajua mtu ambaye alihukumiwa kunyongwa halafu baadaye anaachiwa, ni kitu kinashangaza kwa sababu hakijawahi kutokea, lakini nimeona nifanye hivyo kwa ajili ya Watanzania, Muendelee kusimamia wajibu wenu na kusimamia sheria, mtu anayehukumiwa kufungwa afungwe kweli, na nilishatoa wito kwa magereza, pasiwepo wafungwa wa kukaa tu na kupumzika, wafanye kazi, kufungwa si kustarehe.”amesema Rais Magufuli kwenye taarifa hiyo.

Soma zaidi–Rais Magufuli atoa msamaha kwa Papii Kocha na Babu Seya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents