Soka saa 24!

Rais Magufuli alivyoguswa na kifo cha Dkt Reginald Mengi

Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameeleza kusikitishwa na kifo cha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt Reginald Mengi, na kusema kuwa daima ataukumbuka mchango wake katika Taifa.

Rais Magufuli akiwa Mengi enzi za uhai wake.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Dkt Magufuli ametoa pole kwa wanafamilia na jumuiya wa wafanyabiashara nchini, kutoka na msiba huo mzito.

Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee na rafiki yangu Dkt. Reginald Mengi. Nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Taifa na maono yake yaliyopo katika kitabu chake cha I Can, I Will, I Must. Poleni wanafamilia, wafanyakazi wa IPP na Jumuiya ya Wafanyabiashara, ameandika Rais.

Mbali na Rais, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas amesema kuwa amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa IPP, Mzee Reginald Mengi.

Kama alivyopata kusema yeye mwenyewe siku za uhai wake kuwa watu wanaoacha a

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW