Aisee DSTV!
SwahiliFix

Rais Magufuli alizwa na kifo cha mzee Mugabe ‘Jasiri wa Afrika aliyekataa ukoloni kwa vitendo’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko taarifa za kifo chan baba wa taifa la Zimbabwe, Robert Mugabe.
Image result for rais magufuli na mugabe
Akitoa salamu zake za rambi rambi kufuatia msiba huo mzito, Rais Magufuli amesema kuwa Afrika imepoteza moja ya kiongozi jasiri, Aliyepinga ukoloni kwa vitendo.
Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe, Afrika imepoteza mmoja wa Viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa Afrika na aliyekataa Ukoloni kwa vitendo, Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina”– Ameandika Rais Magufuli kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Rais Mugabe (95) amefariki usiku wa kuamkia leo Septemba 6, 2019 nchini Singapore alikokuwa akipatiwa matibabu kwa muda mrefu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW