Habari

Rais Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero – Waziri Mkuu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefanya ziara katika hospitali ya wilaya ya Ruangwa na amekabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa huku akisema Rais Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo Jumatano hii, alipotembelea hospitali hiyo, ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi ambapo amesema juhudi hizo ni muendelezo wa mkakati wa serikali kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipo kabidhi gari mbili za kisasa za kubebea wagonjwa,katika hospitali ya Wilaya Ruangwa (Picha Ofisi ya Waziri Mkuu)

“Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi kero mbalimbali zinazowakabili zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”

Aidha Waziri Majaliwa amesema magari hayo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake. Huku akisema magari hayo ya kisasa yatasaidia kurahisisha usafiri kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura katika hospitali kubwa.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents