Burudani

Rais Magufuli amjibu Zitto na Wafanyabiashara ‘Serikali ina fedha, tutatumia hata majeshi kununua korosho’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametolea maelezo sakata la zao la korosho ambapo amesema kuwa endapo wafanyabiashara watakataa kununua kwa bei elekezi ya Tsh 3000 kwa kilo.

Image result for rais magufuli
Rais Magufuli

Akizungumza na wafanyabiashara wa korosho Ikulu jana Oktoba 28, 2018  Rais Magufuli amewataka wafanyabiashara kununua korosho kwa bei isiyopungua elfu 3000 na kama watakataa basi serikali ipo tayari kununua.

Kama hamtaki kununua Korosho kwa bei ya maslahi kwa wakulima, Serikali itazinunua kwa bei nzuri na tutazihifadhi, nipo tayari hata kutumia majeshi yetu kununua Korosho na tutatafuta masoko ya uhakika ili tuuze kwa bei nzuri.“amesema Rais Magufuli.

Serikali ina hela, inaweza kununua Korosho za wakulima wa Lindi na Mtwara kwa siku mbili. Tumenunua ndege, tumejenga reli, hatuwezi kushindwa kununua Korosho,“ameeleza Magufuli.

Wakati tamko hilo likijiri hapo jana, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliongelea sakata hilo akitaka serikali itoke hadharani kueleza sakata hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents