HabariVideos

Rais Magufuli amjulia hali na kumshushia maombi mama yake mzazi aliyelazwa Hospitalini Dar (+video)

Rais Magufuli amemjulia hali Mama yake mzazi Bibi. Suzana Magufuli ambaye anapatiwa matibabu Jijini Dar es Salaam tangu miezi mitatu iliyopita baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (Heart Stroke).

Aidha, Rais Magufuli ameongoza maombi ya kumuombea Mama yake pamoja na watu wote wanaokabiliwa na maradhi na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2019.

Vilevile amewashukuru Madaktari na Wauguzi wanaomhudumia Mama yake na wagonjwa wengine nchini na amewaombea kwa Mwenyezi Mungu heri na fanaka katika majukumu yao ya kunusuru maisha ya watu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents