Burudani ya Michezo Live

Rais Magufuli ampigia simu Mwana FA, amuambia anaupenda wimbo wake ‘Dume Suruali’

Rais Dkt John Magufuli ni shabiki wa muziki wa Mwana FA. Na ndio maana ameamua kunyanyua waya na kumpigia simu rapper huyo kumwambia kuwa ni msikilizaji mzuri wa ngoma zake.

Cha kuvutia zaidi, Rais amemweleza FA kuwa wimbo anaoupenda ni Dume Suruali aliomshirikisha Vanessa Mdee.

“Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais @MagufuliJP kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa #DumeSuruali,” ametweet Mwana FA.

“Utoe heRa kwani ina tv ndani?” (in his voice) ????????…,” ameongeza FA.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW