Habari

Rais Magufuli ampoza mkuu wa mkoa wa Arusha kwa simu ya matumaini na pongezi

Baada ya uvumi katika mitandao mbalimbali kuhusu kufanyika utenguzi wa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amempigia simu na kumwambia kuwa awe na amani.

magufuli

Gambo ameyasema hayo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya taarifa kuhusu Rais kutengua uteuzi wake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

4-5

“Kabla ya hapo ziliingia simu kibao, baadaye mheshimiwa rais alinipigia simu,akaniambia kuwa ‘nina full confidence na wewe, I wish you all the best, labda wafikirie promotion hayo mengine hayapo.’ Na baadaye akaniambia ‘ili wajue kwamba nimekwambia, hebu niitie mmoja niongee naye’ ndio akapata nafasi ya kuongea na mheshimiwa rais,” alisema Gambo.

“Lakini meseji yake anasema anawapenda sana, anawajali sana,kikubwa tu anataka mmlipe kodi yake, mfuate sheria na mfuate taratibu na asitokee mtu yeyote kwenye ngazi yoyote kuja kukutisha kwenye haki yako. Amesema sisi sio mabosi wenu ni watumwa wenu,” alisema Gambo akinukuu maneno ya Rais Magufuli.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents