Habari

Rais Magufuli amtaka mzee Museveni aongeze ukali “Kwanini ucheleweshwe na watendaji” (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemshauri Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuongeza ukali kwa viongozi wake ili miradi mikubwa kama ule wa bomba la mafuta la kutoka Hoima hadi Tanga usisue sue.

Rais Magufuli amesema hayo leo Septemba 6, 2019 kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda, Uliohudhuriwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni jijini Dar Es Salaam.

Rais Magufuli amedai kuwa kwa upande wa Tanzania, Serikali imejitolea gharama zote lakini vikwazo vimekuwa kwa viongozi wa mamlaka za kodi nchini Uganda, Ambao ndio wanasababisha mradi huo kuchelewa.

Nimemwambia Rais Museveni, mimi nimebadili makamishina wa TRA watano ndani ya miaka mitatu na nusu, sasa kama TRA yake wanachelewesha kuruhusu ujenzi wa Bomba la mafuta kisa kodi awabadili, unatakiwa kupoteza kidogo ili upate kikubwa’,“ameongea Rais Magufuli na kumtaka Museveni aongeze ukali katika hilo.

Bomba likishaanza makusanyo ya mapato ya Uganda, Uganda kwa takwimu ndio itakuwa nchi inayoongoza kwa uchumi kwa Afrika.. Kwanini ucheleweshwe na watendaji, mzee inawezekana umekuwa mpole, wakati ule ulipokuwa ukipigana ulikuwa mkali!..Sasa uongeze ongeze ukali kidogo kwenye hili,”amesema Rais Magufuli.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents