Habari

Rais Magufuli amteua Kamishna mpya wa TAKUKURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Aidha, taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema kuwa uteuzi huo umeanza leo tarehe 6/ 9/ 2018 ambapo kabla ya uteuzi huo Diwani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Kamishna Diwani Athumani anachukua nafasi ya Kamishna wa wa Polisi, Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa balozi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents