Habari

Rais Magufuli amtumbua Waziri Mwigulu Nchemba, amtaja atakayechukua nafasi yake

Leo Julai 01, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba .

Image result for Mwigulu nchemba na Rais Magufuli
Dkt. Mwigulu Nchemba na Rais Magufuli

Rais Magufuli ametangaza nafasi hiyo kwa sasa kuwa itachukuliwa na aliyekuwa  Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuziba nafasi hiyo.

Mnamo tarehe 11 Juni 2016 Rais Magufuli alimteua Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akitokea kwenye Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Tazama video ya uteuzi huo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents