Habari

Rais Magufuli amtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa DR Congo, Felix Tshisekedi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za pongezi Rais Mteule wa DR Congo, Felix Tshisekedi kwa kutangazwa na mahakama nchini humo kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya urais kwenye uchaguzi uliofanyika Desemba 30, 2018.

Image result for rais magufuli amtumbua
Rais Magufuli

Rais Magufuli ametuma salamu hizo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ikiwa ni siku moja imepita tayari tangu Mahakama nchini humo, kufuta malalamiko ya baadhi ya wagombea wenza wa Tshisekedi kudai kuwa matokeo ya uchaguzi yaligubikwa na wizi.

Felix Tshisekedi anakuwa Rais wa kwanza kutoka katika chama cha upinzani nchini humo, na ameshinda kwa asilimia 38 ya kura zote zilizopitwa kwenye uchaguzi huo.

Soma zaidi –http://bongo5.com/felix-tshisekedi-atangazwa-rasmi-na-mahakama-kuwa-rais-mteule-wa-dr-congo-01-2019/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents