Habari

Rais Magufuli apandisha cheo maofisa wa uhamiaji

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewapandisha cheo maofisa sita wa Uhamiaji kuwa makamishna wa Uhamiaji na kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi la Uhamiaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, kupandishwa vyeo na uteuzi huo umeanza tangu Februari 28, mwaka huu.

Aliwataja walioteuliwa kushika nyadhifa hizo ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka na Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Musanga Etimba kuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hannerole Manyanga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa Rais Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Mourice Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents