Habari

Rais Magufuli apiga ‘STOP’ Polisi kufyeka bangi (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza IGP, Simon Sirro kutowaagiza Polisi kufyeka mashamba ya bangi badala yake watumie nji za intelijensia kuwakamata wahusika na ikishindikana wakamate kijiji kizima wafyeke mpaka atakapo tajwa muhusika.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa nyumba za Jeshi la Polisi mkoani Arusha ambapo amesema hilo ndio jambo linalomkera.

“IGP mimi kuna kitu kinaniudhi jinsi polisi wanavyoenda kukata bangi hamkuajiriwa kukata bangi, kama bangi iko kijiji fulani shika kijiji kizima wazee na wakina mama wakafyeke bangi,” amesema Rais Magufuli.

“Askari wasiende kufyeka bangi. Hawakuajiriwa kufyeka bangi, usiwatume Maaskari wako kufyeka bangi, mtaumwa nyoka mle mna uniform nzuri, msidhalilishe jeshi kwa kufyeka bangi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents