AwardsHabari

Rais Magufuli ashinda tuzo nchini Ghana ya kiongozi bora barani Afrika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameshinda tuzo ya The African Prestigious Awards 2017 kwenye kipengele cha kiongozi bora wa bara la Afrika.

Tuzo hizo ambazo zimetolewa Aprili 14, 2018 Wikiendi iliyopita jijini Accra nchini Ghana pia zilishuhudia Watanzania wengine watatu katika tasnia ya filamu wakiibuka washindi.

Waigizaji hao ni Monalisa na Ray Kigosi waliyoibuka washindi kwenye vipengele vya Muigizaji bora wa kike barani Afrika na Muigizaji bora wa kiume barani Afrika.

Na mwingine ni mpiga picha Moiz Hussein ambaye ameshinda tuzo ya mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.

Soma zaidi – Monalisa, Ray Kigosi washinda tuzo nchini Ghana

Unaweza kutazama washindi wengine kwenye website ya waandaaji wa tuzo hizo HAPA,Pia kufuatia tuzo hiyo msemaji wa serikali amempongeza Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents