Rais Magufuli ataja sababu za kuchelewesha Baraza la Mawaziri, wale wa kwenda kwa waganga waende (+Video)

Rais wa Tanzania John Magufuli hii leo amemuapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa awamu ya pili , Prof Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki na Dkt Philip Mpango Waziri wa fedha na mipango.

Watatu hao wameapishwa leo mjini Dodoma, huku Rais Magufuli akieleza sababu za mchakato wa kuunda baraza la mawaziri kuwa wa polepole kuliko ilivyotarajiwa na wengi.

Rais Magufuli amesema hana haraka sana ya kuteua baraza la mawaziri.

“Mwaka huu, tuna wabunge zaidi ya 350 na bado wabunge wa nafasi zile kumi wa mimi kuteua, sikutaka niteue haraka haraka. Mwaka 2015 ilikuwa rahisi kwasababu idadi ya wabunge wa CCM ilikuwa ndogo”

Dkt Magufuli ameeleza umuhimu wa kuwa na Waziri wa fedha kwa kuwa zinahitajika na kwamba haziwezi kusubiri kwa miezi mitatu..minne

”Si kwamba hawa wawili ni maarufu sana kuliko waliobaki, miaka ya nyuma niliwateua hawakuwa na majimbo, na niliwaambia waende kwenye majimbo au waende huko walikotoka, wakaenda kwenye majimbo.” Alisema Magufuli

”Lakini kwa sababu niliona kuwa nitachelewa kidogo kuwa na baraza la mawaziri na ninyi waheshimiwa wabunge lazima mlipwe mishahara na posho zenu na lazima tutafue fedha za kulipa mishahara wafanyakazi na watanzania na lazima tuendelee kuwa na miradi ya maji na barabara ambayo haisimami”

Rais Magufuli amewataka wabunge watulie huku yeye akifanya mchakato wa kuteua baraza la mawaziri huku akiwatania wabunge kuwa wale wa kwenda kwa waganga waende na baadaye akasema anajua wabunge wetu wanaongozwa na mungu anatumai watenda misikitini na makanisani na sio kwa waganga.

https://www.youtube.com/watch?v=rifXU-C9sss&t=7199s

https://www.youtube.com/watch?v=rifXU-C9sss&t=7199s

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW