Habari

Rais Magufuli atoa mkono wa Eid El Fitri kwa makundi maalum

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa mkono wa Eid El Fitri zenye thamani ya shilingi 10,922,000 kwa vituo 9 vya Mkoa wa Dar es Salaam, vituo 2 vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.

Zawadi hizo zimekabidhiwa leo katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga Jijini Dar es Salaam na Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya Ustawi wa Jamii, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Simon Panga kwa niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.

Panga amezitaja zawadi zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo kwa watu wengi.

“Mhe. Rais kwa upendo wake wa dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na wazee wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa katika makazi, katika kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri mwaka 2017,” amesema Panga.

Aidha, amevitaja vituo vilivyonufaika na zawadi za Mhe. Rais kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN Kathry- Ilala, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima Chakuwama, Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke, Makao ya Watoto Yatima Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization), Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam – Upanga, Makazi ya Wazee na Wasojiweza Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya Watoto Wenye Ulemavu Yombo.

Na Emmy Maipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents