Habari

Rais Magufuli atoa msamaha kwa wafungwa 8,157

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 8,157 huku wafungwa 1828 watatolewa leo.

Akizungumza leo katika maadhimisho ya Miaka ya 56 ya Uhuru, Rais Magufuli huku akisema kuwa watu 6,329 watapunguziwa muda wa kukaa jela.

“Ninatoa msamaha kwa wafungwa 8,157 na wafungwa 1,828 watatoka leo na 6,329 watapunguziwa muda wa kukaa jela,” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alieleza kuwa amesamehe watu 61 waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents