Tupo Nawe

Rais Magufuli atoa siku 5 kwa DC Nkasi na RPC Rukwa walipe Tsh. Mil 15 kwa mama aliyeibiwa ng’ombe (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi mkoani humo, Kulipa Tsh. Milioni 15 kwa mama aliyetoa malalamiko kwake kuwa aliibiwa Ng’ombe 25 na mwizi wake akaachiwa huru na Askari Polisi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Oktoba 8, 2019 akiwa kwenye ziara yake ya mwisho Wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Hii ni baada ya mama mmoja aliyejitokeza kutoa malalamiko yake kwenye mkutano wake wa hadhara.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW