Shinda na SIM Account

Rais Magufuli atua Uganda, akutana na Museveni Ikulu ya Entebbe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewasili nchini Uganda kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakao fanyika Ijumaa hii ya February 23 mjini Kampala.

Rais Magufuli amepokelewa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebbe, na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mhe. Sam Kutesa na kuelekea katika Ikulu ya Entebbe kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Museveni.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW