Habari

Rais Magufuli atumbua vigogo Kagera waliotaka kuzitafuna fedha za waathirika wa tetemeko

Operesheni ya kutumbua majipu bado inaendelea. Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa mkoa wa Kagera, Amatusi Msole na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Steven Makonda baada ya kubainika kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki na kutumia jina la akaunti rasmi ya kuchangia tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.

tpa23

Kwenye taarifa hiyo iliyosomwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa imesema kuwa Rais Magufuli amemtumbua Mhasibu Mkuu wa mkoa wa Kagera, Simbaso Swai na kuvitaka vyombo vya usalama kulifuatilia jambo hilo na kuwatia hatiani wote waliohusika kufungua akaunti hiyo.

Wakati huo huo serikali ya India kupitia kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi imetoa msaada wa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kusaidia maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Jumamosi ya Septemba 10, mwaka huu.

“Serikali na wananchi wa India wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa maafa hayo yaliyosababisha vifo vya watu na uharibifuwa mali,” imesema taarifa hiyo.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemshukuru Waziri Mkuu huyo na serikali yake kwa kutoa mchango huo pamoja na salamu za rambi rambi na amesema serikali yake imeguswa na moyo wa upendo waliouonyesha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents