Habari

Rais Magufuli avutiwa na muziki wa Harmonize ‘Natamani akagombee ubunge Tandahimba’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli anatamani kumuona msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Harmonize akigombea Ubunge kwenye jimbo analotoka la Tandahimba.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jana Oktoba 15, 2019 wakati akifanya mkutano wa hadhara mjini Ruangwa mkoani Lindi ambapo Harmonize alitumbuiza kwenye mkutano huo.

Nawapongeza sana waimbaji hawa wakina baba, lakini nampongeza sana Harmonize (Rajab Abdul) sijui anatoka jimbo gani? amesema Rais Magufuli “Anatoka jimbo gani huyu? Tandahimba? Mbunge wa kule ni nani?” Amehoji Rais na kueleza, “Aaa ningetamani kweli Harmonize akagombee kule akawe mbunge wa Tandahimba”.

Kwa sasa jimbo la Tandahimba lipo chini ya Mbunge wa (CUF), Ahmad Katani, Hivyo huenda mwakani Harmonize akatupa karata kwenye siasa kwa kugombea jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.

Harmonize ni moja ya wasanii wa Bongo Fleva ambaye amekuwa akipewa nafasi ya kutumbuiza katika mikutano mbalimbali ya hadhara anayofanya Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents