Habari

Rais Magufuli awapa mtego wakuu wilaya na wakuu mikoa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa serikali haitatoa chakula kwa sehemu itakayokumbwa na njaa huku akiwataka Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa watakaoshindwa kuhamasisha kufanya kazi kiongozi wananchi huyo hafai hiyo amewataka kutafuta kazi nyingine.

Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo akiwa katika ziara mkoani Singida na leo amezindua barabara ya Manyoni – Itigi – Chaya yenye urefu wa KM 89.3.

“Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa sitoi chakula kama kwako kuna njaa. Wilaya ikiwa na njaa nitajua wewe mkuu wa mkoa hufai, mkuu wa wilaya hufai. Mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya atakayeshindwa kuwahamasisha watu wake wafanye kazi, hafai kuwa kiongozi. Tuwahamasishe wananchi kulima wenyekiti wa vijiji wahamasishe wananchi kulima,viongozi wote wahamasisheni wananchi kilimo,” amesema Rais Magufuli.

“Ikiwezekana na wewe Mkuu wa wilaya au Mkoa, kama unakaa kijijini au ni Katibu Kata onyesha mfano wako wa kazi. Ukiwa Diwani hivyo hivyo, ukiwa mbunge hivyo hivyo. Ndiyo maana ninatimiza wajibu wangu wa kuhamasisha watu, chapa kazi.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents