Habari

Rais Magufuli awapiga vijembe upinzani adai CCM itatawala milele na ‘watapata tabu sana’

Rais Magufuli awapiga vijembe upinzani adai CCM itatawala milele na 'watapata tabu sana'

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, amesema kuwa Chama hicho kitaendelea kutawala na kitatawala milele kwani ndio chama pekee kinacholeta amani na maendeleo.

Rais Magufuli kushoto akiweka jiwe la Msingi la Chuo cha Uongozi cha Mwl. Julius Nyerere kilichopo mkoani Pwani.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Julai 16, 2018 huko mkoani Pwani wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa chuo cha uongozi cha Mwl. Julius Nyerere kilichopo Kibaha ambacho ujenzi wake umegharimu tsh. Bil 100 kwa ufadhili kutoka chama cha CPC cha nchini China.

“CCM ni chama tawala na kitaendelea kutawala milele na milele, wanaohangaika watapata tabu sana. Chama hiki kipo na kitaendela kuwepo na kitaendelea kuleta maendeleo kwa ajili ya Watanzania hakuna mbadala ni CCM, CCM, CCM mpaka milele. Kwa wananchi na wanachama wapenda Chama cha Mapinduzi endeleeni kutembea kifua mbele, tumeamua kuleta Tanzania ya kisasa, Tanzania yenye maendeleo, Tanzania yenye viwanda, Tanzania yenye muelekeo, Tanzania inayoshirikiana na nchi nyingine katika Afrika. Tanzania inayowapigania wananchi hasa wanyonge ili waweze kushiriki maendeleo yao. Tanzania inayopinga rushwa, Tanzania inayopinga unyonyaji,“amesema Rais Magufuli.

China kupitia Chama chake Tawala cha CPC kinatoa ufadhili kama huo kwa vyama sita vya ukombozi barani Afrika ikiwemo CCM vingine ni ANC-Afrika Kusini, ZANU-PF-Zimbabwe, Frelimo-Msumbiji, MPLA-Angola na SWAPO-Namibia.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents