Habari

Video: Rais Magufuli awasili mkoani Kilimanjaro

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewasili mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu, ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe ya wafanyakazi ‘Mei Mosi’.


Picha na Michuzi

video:

Ijumaa hii Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Magufuli pamoja na kushiriki sherehe hizo.

Aidha Mkuu wa mkoa huyo, alisema ni bahati kubwa kwa mkoa huo kutembelewa na mheshimiwa Rais kuja kuungana na wafanyakazi pamoja na wananchi, katika kuadhimisha sherehe hizi za wafanyakazi. Mbali na hilo Rais huyo atafanya kikao na viongozi wa dini wa mkoa huo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents