Habari

Rais Magufuli awataka Watanzania kuchangamkia fursa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewataka Watanzania kuchangamkia fursa kwenye mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale-Uganda hadi Tanga-Tanzania.

Rais Magufuli amesema mradi huo ni kielelezo tosha cha muendelezo wa ushirikiano wa nchi zetu mbili.

“Nchi yetu imepata mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale/Uganda hadi Tanga/Tanzania,ni fursa kubwa ktk kuujenga uchumi wetu. “Mradi huu ni kielelezo tosha cha muendelezo wa ushirikiano wa nchi zetu mbili na hasa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki,” Rais Magufuli alitweet.

“Wito wangu kwa watanzania wote ni kuchangamkia fursa hii kipindi cha ujenzi na uendeshaji wa mradi huu. Mungu Ibariki Tanzania.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents