Rais Magufuli awataka Watanzania wasiogope kuzaliana ‘nchi yetu imekuwa ya mfano’

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewaasa Watanzania kuwa wasiogope kuzaliana kwani nchi ikiwa na watu wengi inakuwa na sauti kwenye jumuiya.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli

 

Akihutubia kwenye  uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kiwango cha Standard Gauge kutoka Morogoro mpaka Makotopora, Dodoma, amesema kuwa tatizo sio kuwa na watu wengi katika nchi bali kinachotakiwa ni kila Mtanzania kuchapa kazi na kisha kutolea mfano wa nchi ya China.

“Hivi karibuni tumeambiwa sasa Watanzania tumefika milioni 55 wapo waliosema kwamba kwanini milioni 55? tunazaana mno, mimi nasema tuzaliane zaidi. Nchi ya Uchina ina watu bilioni 1.3 na ndio maana sasa hivi nchi ya uchina ipo uchumi wake upo juu, lakini mnapokuwa wengi mnakuwa na sauti hata kwenye Block mlizo nazo, sisi tupo kwenye block ya East Afrika Community  sisi tupo watu milioni 55  idadi ya watu wetu ni sauti tosha, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki,”amesema Rais Magufuli na kusisitiza.

Kinachotakiwa ni sisi Watanzania tuchape kazi  suala si kuwa wengi suala ni namna gani hao Watanzania wanashiriki katika kuleta maendeleo ya nchi yao. Nchi ya Denmark ina watu milioni 5 lakini kwa sababu ya uchapakazi wao  imekuwa ikitoa misaada mpaka kwenye nchi kama Tanzania yenye watu milioni 55, kwahiyo jukumu letu tulilonalo ndugu zangu tusiogope kuwa wengi, tukubali kuwa wengi lakini wengi wanaochaopa kazi,“amesema Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema nchi ya Tanzania kutokana na ukuaji wake wa uchumi na fursa za ajira zinavyoongezeka.

Kwa mafanikio haya makubwa ambayo yameanza kupatikana katika nchi yetu, Nchi yetu imeanza kuwa ni nchi ya mfano na ndiyo maana hata Mheshimiwa balozi hapa (Balozi wa Uturuki) amezungumza, ameeleza hapa jinsi Tanzania inavyosifiwa, Hii reli hakuna nyingine wapo wengine wamejaribu lakini wamejenga ya hovyo hovyo tu,“amesema Rais Magufuli.

 

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW