Habari

Rais Magufuli kutua Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli Jumatano hii anatarajiwa kutinga jijini Arusha kwa ziara ambapo mapema asubuhi atafungua barabara ya Kami kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi Mererani wilayani Simanjiro.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kupokewa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro KIA asubuhi saa mbili.

“Napenda kutumia fursa kuwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Septemba 23 kuanzia saa 12:30 asubuhi,” alisema Gambo.

Gambo amesema baada ya kupokelewa atakwenda Mererani Mkoa wa Manyara kuzindua barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa kilomita 26.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents