Habari

Rais Magufuli kwenye ujenzi wa daraja ‘Naomba mradi ukamilike nikiwa madarakani, atakayekuja anaweza kuja kuufuta huu mradi’ – Video

Rais Magufuli kwenye ujenzi wa daraja 'Naomba mradi ukamilike nikiwa madarakani, atakayekuja anaweza kuja kuufuta huu mradi' - Video

Rais Magufuli ameeleza kuwa alifanya juhudi za makusudi kwa kumtumia Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tanroads, Patrick Mfugale, kukamilisha mchoro wa daraja la juu kwenye ziwa Victoria eneo la Kigongo Busisi lenye urefu KM 3.2.

Akiongea katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi leo Desemba 7, 2019, Rais Magufuli amesema, mradi huo ni muhimu na anamshukuru Mfugale kwa kukamilisha mpango mapema pamoja na Bunge kwa kupitisha bajeti ya ujenzi huo.

‘Nimeona nimtumie Mfugale haraka haraka, nikamwambia kamilisha mapema katika kipindi changu cha Urais inawezekana muda wangu ukiisha anaweza akaja Rais mwingine akaufuta huu mradi, na huyu Mfugale amekuwa akifanya vizuri katika miradi yote ya madaraja nchini’, ameeleza.

Aidha Rais Magufuli amewaasa wananchi wa Mwanza hususani wa Wilaya za Sengerema na Misungwi ambapo mradi huo upo kuutumia vizuri kwa kunufaika kiuchumi kwani ni mradi muhimu kwa watanzania wote na nchi jirani.

Awali Mfugale alieleza kuwa mradi huo unagharimu Shilingi Bil. 699, ambazo zote ni fedha za ndani na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 40.

Mwanafunzi alivyomkosha Rais Magufuli na kumkabidhi milioni 5.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents