Habari

Rais Magufuli na wananchi wa Njombe wafanya sala ya toba mauaji ya watoto, amrejesha OCD aliyemtumbua (Video)

Rais Magufuli amemtumbua na kumrudisha kituo cha kazi OCD wa Njombe alasiri hii ya leo baada sala ya toba iliyofanyika kwa kushindwa kuzuia mauaji ya watoto mkoani humo.

Tukio hilo limetokea leo wakati Rais Magufuli akiwa kwenye ziara mkoani Njombe alieleza kuwa, “huwezi ukawa RPC na bado watoto wa wenzako wanapotea umekaa tu ofisini na nyota zako mbona mtoto wako hawajapotea?. Kuanzia sasa hivi OCD wa hapa sio OCD tena, najua upo hapa unanilinda”.

Akikazia kuhusu msimamo wake kwenye mauaji ya Njombe Rais Magufuli alimuonya Mkuu wa Mkoa na Wilaya huku akitaka wajitathmini

“Na hili suala la watoto kuuawa likijitokeza tena ujue kuwa mtaondoka wote kuanzia RC, ma DC, wenyeviti mpaka Mwenyekiti wa CCM Mkoa, wananchi wa Njombe acheni imani potofu za kishirikina”.

“Njombe mmelitia doa taifa, kwa hili naomba tufanye toba watanzania wote nikiwemo na mimi ninayeongoza watanzania wanaoua wenzao”, ameongeza

Baada ya toba

Muda mfupi baada ya kumalizika kwa toba, Rais Magufuli amesema. “nimeamua kumsamehe OCD haya rudi kazini. Yuko wapi?”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents