Habari

Rais Magufuli umeisafisha CCM na kuivua gamba – Afande Sele

Rapa mkongwe nchini Tanzania, Afande Sele baada ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi(CCM) Mapema leo amemwambia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa amekisafisha chama hicho na kukivua gamba tofauti na kilivyokuwa hapo awali.

Afande Sele ameyasema hayo leo Machi 15, 2018 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza sigara cha Philips Moris International mjini Morogoro kilichozinduliwa na Rais Magufuli.

“Rais chama chako cha mapinduzi umekisafisha umekivua gamba nani chama ambacho kimerudi katika uimara wake kama chama cha wanyonge, kwa jinsi ambavyo Mhasisi wetu baba wa Taifa alitaka kiwe ndivyo ambavyo umekifanya chama cha mapinduzi leo, Mh. Rais naomba nikupongeze sana kwa hilo lakini kama haitoshi nikuhakikishie kwamba nimeamua kujiunga upande mmoja na wewe ili nisiachwe na jahazi hili,” amesema Afande Sele.

“Kwasasa hivi Tanzania kama dereva gari limetulia na linakwenda na mimi kama abiria niache ninywe soda yangu kwa furaha na amani, kwasababu naamini chombo chetu kinakwenda salama na sipendi kesho historia inihukumu niwe miongoni mwa wale ambao hawakuchangia chochote.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents