Habari

Rais maskini zaidi duniani akataa malipo ya uzeeni

Aliyekua rais wa Uruguay, Jose Mujica ambaye alifahamika kama rais maskini zaidi duniani amesema hatachukua malipo yake ya uzeeni tangu aanze kuhudumu kama seneta.

Mujica aliacha kazi ya useneta siku ya Jumanne kiti ambacho amekua akishikilia tangu muda wake wa kuhudumu kama raisi ulipo kamilika mwaka 2015.

Kwa mujibu wa BBC rais huyo mstaafu alidai kuwa amechoka na hangeweza kuendelea na kazi hadi mwaka wa 2020. Muasi huyo wa zamani wa mlengo wa kushoto ana miaka 83.

Mujica aliwasilisha barua ya kuacha kazi kwa mkuu wa seneti. Alisema kwamba fikra ya kuacha kazi ni ya kibinasfi huku akiongeza kuwa ni uchovu wa safari ndefu.

Hata hivyo aliongeza kua ataendelea kuchangia hoja kwa sababu bado akili yake inafanya kazi. Mujica anayejulikana kwa matamshi yake ya kichesi aliomba msamaha kwa wenzake kwa uamuzi huo.

Mwaka 2016, alidai rais wa Venezuela Nicolás Maduro ni mwendazimu kama mbuzi. Umaarufu wake ulienea kutokana na maisha yake ya chini ya kukataa kuishi kwenye Ikulu ya rais.

Wakati akiwa rais na hata sasa yeye pamoja na mkewe ambaye pia alimsaidia katika vita vya msituni wamekua wakiishi katika shamba moja nje kidogo mwa mji wa Montevideo.

Alitoa mshahari wake kwa misaada na kile alichobaki nacho tu alipoingia ofisini mwaka wa 2010 ni gari aina ya Volkswagen Beetle la mwaka 1987.

Gari hilo lilipata umaarufu na mwaka 2014 alipewa dola milioni moja lakini akakataa huku akidai kuwa atashindwa kumbeba mbwa wake mwenye miguu mitatu.

Kuacha kazi kwa Mujica hakukupokelewa na mshangao kwa sababu alikua amedokeza kufanya hivyo mnano Agosti 3 alipofika mara ya mwisho seneti.

Wakati huo, mahasimu wake wa kisiasa walisema hawakua na uhakika ya kwamba atastaafu. Seneta Luis Alberto Heber alidai kuwa Mujica aliacha kazi ili ajipange kuwania kiti cha urais mwaka 2019 kwa mara ya pili.

Huku wenazke katika seneti wakimjalia mazuri wakosoaji waliendeleza mijdala kwenye mitandao ya kijamii wakidai aombe msamaha vitendo alivyofanya wakati akiwa mwanachama wa waasi wa Tupamaros miaka ya 1960 na 70.

Related Articles

13 Comments

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents