Burudani ya Michezo Live

Rais mpya Malawi, Lazarus Chakwera aapishwa

Rais mpya wa Malawi Mhe.Lazarus Chakwera ameapishwa hii leo huku hafla ya kuapishwa kwake ikifanyika katika mji mkuu wa Lilongwe baada ya kiongozi huyo kushinda katika uchaguzi wa marudio uliofanyika nchini humo.

Lazarus Chakwera ameshinda uchaguzi  wa  wiki  hii  wa  rais ulioamriwa  kufanyika  tena kwa asilimia 58.57 ya kura, tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imesema.

Malawi Opposition Lazarus Chakwera (Reuters/E, Chagara)

Ilikuwa  ni  mabadiliko  makubwa ya majaaliwa  kwa  kiongozi aliyeko madarakani, Peter Mutharika, ambaye  ushindi  wake  katika uchaguzi  wa  mwezi  Mei  2019 ulibatilishwa na mahakama  ya katiba, yakihusishwa  na  udanganyifu  mkubwa.

Kiasi ya  wapiga  kura  milioni 6.8  katika  taifa  hilo  dogo  la  kusini mwa  Afrika walijitokeza  katika  vituo vya  kupigia  kura  siku  ya Junanne. Na  jana  Jumamosi , tume  ya  mwenyekiti  wa  tume  ya uchaguzi  Chifundo Kachale aliwaambia  waandishi  habari; “Tume imemtangaza Lazarus Chakwera , kwa  kupata  asilimia 58.57 ya kura, kuwa  amechaguliwa  kuwa  rais wa  Malawi.

Malawi Präsident Peter Mutharika PK Wahlen (picture-alliance/AP Photo/T. Chikondi)

Mutharika  alikuwa  wa  pili  kwa  kupata  kura  1,751,377, wakati mgombea  ambaye  hajulikani  sana  Peter Dominico Kuwani amepata  kuwa 32,456.

Watu waliojitokeza  kupiga  kura  ni  asilimia 64.81.

Tangazo  hilo lilipokelewa  kwa  shangwe  kubwa  na  vigelegele wakati  waungaji  mkono  upinzani  wakipepea  bendera  ya  Malawi yenye rangi  nyekundu , nyeusi  na  kijani na  kuimba “serikali” katika lugha  ya  Kichechewa.

Mwezi  Februari , mahakama  ya  juu  ya  Malawi  iliona  kuwa uchaguzi  wa  kwanza  umegubikwa  na  mapungufu  mengi , ikiwa  ni pamoja  na  matumizi ya  wino wa  kufanyia  marekebisho kubadilisha  matokeo  katika  karatasi  ya  matokeo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW