Uncategorized

Rais Mstaafu Benjamin Mkapa atangaza kujiuzulu nafasi ya usuluhishi Burundi

Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa amefikia maamuzi ya kujiuzulu nafasi yake kiongozi wa jopo la usuluhishi wa mgogoro wa Burundi aliyoteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2016, na kuishtumu Jumuiya hiyo kushindwa kuunga mkono jitihada.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya Ufaransa (RFI), Baada ya marais wa Uganda, Kenya na Tanzania kukabidhiwa majukumu na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea na mazungumzo na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, kutafuta njia ya kuondokana na mgogoro nchini Burundi, Mwezeshaji huyo, Benjamin Mkapa ameamua kujiuzulu kwenye nafasi yake usuluhishi.

Januari 31, Benjamin Mkapa aliwasilisha ripoti ambayo ilikuwa bado ni siri kwa viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo Benjamin Mkapa amesema, “Serikali na upinzani wanapaswa kuzungumza na kukubaliana kuhusu mfumo wa kisheria na taratibu zinazohitajika kufanyika kwa uchaguzi ujao.

Rais mstaafu wa Tanzania ameelezea masikitiko yake na hatua ya serikali ya Burundi kususia kikao cha mwisho cha mazungumzo na hali hiyo inaonyesha “msimamo wa muda mrefu ” wa viongozi wa Burundi wa kutoshiriki katika mazungumzo baini ya Warundi, aliandika Mkapa.

Lakini hasa Benjamin Mkapa amesikitishwa kuona hakuungwa mkono vya kutosha katika jitihada zake, kwanza na Jumuiya ya Afrika Mashariki: “kutofanyika kwa mkutano wa kilele kuhusu mgogoro wa Burundi ulisababisha mimi kukosa uungwaji mkono wa jumuiya,” amesema rais mstaafu wa Tanzania.

Bw Mkatapa ametoa wito wa kuepo kwa mazungumzo yatakayo washirikisha wadau wote kwa kufuatisha ajenda iliyowekwa katika mazungumzo ya awali na ameomba viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushinikiza uungwaji mkono kwa mchakato wa uchaguzi kwa kuweka masharti kwa uchaguzi wa kuaminika.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents