Habari

Rais Mugabe na mkewe wakalia ‘kuti kavu’ Zanu-PF

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe na mke wake, Grace Mugabe wamekalia kuti kavu na kudondoka ghafla katika nyadhifa ndani ya chama tawala cha Zanu- PF nchini humo.

Rais Mugabe na Mkewe wakiwa katika furaha kipindi cha utawala wao.

Mapema leo mchana nchini humo kwenye kikao cha kamati kuu cha Chama hicho kimefikia maamuzi ya kumvua Rais Mugabe wadhifa wa kiongozi mkuu wa Chama cha Zanu-PF na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Makamu wake wa Rais, Emmerson Dambudzo Mnangagwa huku mke wake Grace Mugabe akivuliwa uanachama wa Chama hicho.

Hayo yamejili baada ya hali ya sintofahamu inayoendelea nchini kuhusu mtikisiko wa kisiasa na uchumi nchini humo.

Pitia yaliyoafikiwa kwenye kikao hicho maalumu kama yalivyochapishwa na ukurasa rasmi wa Twitter wa Chama cha Zanu PF.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents