Michezo

Rais Museveni aitaka Uganda ‘The Cranes’ waifunge Taifa Stars, Zitto Kabwe amjibu

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa licha ya timu yake ya taifa maarufu kwa jina la ‘The Cranes’ kufuzu kushiriki michuano ya Afcon hapo mwakani lakini lazima ihakikishe inapata ushindi kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania.

Museveni ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa  kijamii wa Twitter, ”Hata kama ‘the Cranes’ tayari mmeshafuzu, nafahamu kwamba bado mna mchezo mmoja wa kucheza dhidi ya Tanzania. Tafadhali hakikisha hampotezi kwenye mchezo huo. Pongezi kwa mara nyingine,” amesema Museveni.

Mara baada ya ujumbe huo wa Museveni, naye mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akaandika ujumbe wa kumtaka Rais huyo kuwa na ubinadamu kwakuwa timu yao tayari imeshafuzu.

”Mzee acha roho mbaya. Mmeshasahau mafuta yenu yanapita Tanzania? Shauri yako,” ameandika Zitto Kabwe.

Hii ndiyo rekodi ya Amunike ndani ya Taifa Stars na mambo 10 usiyafahamu

Katika mechi yake ya kwanza timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ alifanikiwa kutoka sare tasa ya bila kufungana 0 – 0 dhidi ya Uganda maarufu kama ‘The Cranes’ ambao walikuwa nyumbani.

Stars iliyopo kundi ‘L’ chini ya Mnigeria huyo ilijikuta ikipata kipigo cha mabao  3 – 0 mbele ya Cape Verde ugenini. Kisha kupata ushindi wa 2 – 0 kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Cape Verde jijini Dar es Salaam.

Ikapoteza na Lesotho  kwa bao 1 – 0 mchezo uliyopigwa wikiendi hii iliyopita siku ya Jumapili.

Msimamo wa kundi hilo Uganda inaongoza kwa kuwa na pointi 13, Taifa Stars alama tano, Lesotho alama tano, na Cape Verde alama nne.

Kwa msimamo huo Uganda ishafuzu, ili Stars apate nafasi ya kwenda Afcon mwakani nchini Cameroon italazimika kuifunga Uganda mchezo wa marudiano Machi 22 uwanja wa Taifa, huku ikiomba Cape Verde  iifunge Lesotho.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents