Burudani ya Michezo Live

Rais Salva Kiir amtumbua Waziri wa mafuta Sudan Kusini, amtaja atakayechukua nafasi yake 

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemfuta kazi mkuu wa wizara muhimu ya mafuta ambayo inaingiza zaidi ya asilimia 90 ya mapato ya serikali ya Sudan Kusini. Kiir alichukua hatua hiyo Alhamis kumfuta kazi Ezekiel Lol Gatkuoth baada ya kuongoza wizara hiyo kwa miaka mitatu na nafasi yake kuchukuliwa na Awow Daniel Chuang.Image result for Ezekiel Lol Gatkuoth

Aliyekuwa Waziri wa Mafuta Sudani Kusini, Ezekiel Lol Gatkuoth 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sauti ya America (VOA), Hata hivyo Rais Kiir hakutoa sababu za kufanya mabadiliko hayo lakini mchambuzi wa kiuchumi anayeishi mjini Juba alieleza inaonekana Gatkuoth alifukuzwa kazi kwa sababu hakuwa muwazi kuhusu namna fedha za wizara hiyo zilivyokuwa zikitumika na huwenda amevunja sheria kuhusu namna ya kuweka fedha ndani ya akaunti kwenye benki moja ya serikali.

Naye mchambuzi wa sera Augustino Ting Mayai wa taasisi ya SUDD yenye makao yake Juba alieleza kwamba katika mwaka wa kwanza wa Ezekiel Lol Gatkouth kama waziri wa mafuta, uzalishaji mafuta na mapato ni kwamba mapato ya serikali yalipungua wakati mzozo ulipokuwa unaendelea nchi nzima pale bei ya mafuta iliposhuka kwenye soko la kimataifa.

Awow Daniel Chuang ndiyo ametajwa kuwa Waziri mpya wa mafuta na madini kufuatia mabadiliko hayo yaliyofanywa na Rais huyo wa Sudani Kusini, Salva Kiir Mayardit

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW