Habari

Rais Shein atoa onyo kali kwa Mawaziri wake, ‘wanayoyatafuta wakitaka watayapata’

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein ametoa onyo kali dhidi ya viongozi wa Baraza la Wawakilishi ambao hawakufika katika mkutano wa ufunguzi wa ziara yake ambayo imeanza rasmi leo katika Wilaya ya Mjini.

“Baadhi ya Mawaziri wangu hawapo, narudia tena leo. Nataka niwaone mawaziri wangu katika ziara hii, wapo wawili wameniaga, wengine hawajaniaga. Nilisema juzi pale Tunguu, narudia tena hii siyo ziara ya mchezo, hii ni ziara ya kazi, wanayoyatafuta wakitaka watayapata,” amesema Shein.

Katika mkutano huo Rais Shein amepokea ripoti ya maendeleo iliyowakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohamed Mahmoud kuhusiana na maendeleo yanayofanyika katika Mkoa wake.

Mkutano huo umewajumuisha viongozi mbalimbali wa serikali, wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wa dini katika Ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi.

Na Laila Sued na Salum Kaorata

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents