Rais Trump ashambuliwa mitandaoni kwa kukosea Kiingereza, mwenyewe ajitetea na kuwazodoa wanaomsahihisha
Rais wa Marekani, Donald Trump amejikuta akishikwa na hasira baada ya wanaharakati mitandaoni kumsahihisha makosa ya kisarufi (grammatical Error) na kimaandishi (Typing error) kwenye Tweets zake huku wakimkebehi kuwa hajui hata kuandika kwa ufasaha kwa lugha ya Kiingereza.
Trump ambaye jana Julai 04, 2018 alitwiti mara moja na kisha kufuta twiti hiyo baada ya kushambuliwa kuwa alikosea kuandika, huku akidai mtandaoni kuna vyombo vya habari ambavyo haviangalii anachokifanya bali vinaangalia makosa yake ya kisarufi (grammatical error) mtandaoni.
“Nimeshawahi kuandika vitabu bora na vilivyouzwa zaidi, kwa hiyo huwezi kunipima kamwe kwenye uwezo wangu wa kuandika. Hii inaonesha wazi kuwa kuna vyombo vya habari vinatoa habari bandia (Feki) kwa kutumia muda mrefu kutafuta makosa kwenye tweet zangu,“ameandika Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.
After having written many best selling books, and somewhat priding myself on my ability to write, it should be noted that the Fake News constantly likes to pore over my tweets looking for a mistake. I capitalize certain words only for emphasis, not b/c they should be capitalized!
— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) July 3, 2018
Hata hivyo wataalamu wa lugha waliendelea kumshambulia Trump kuwa bado Tweet hiyo ilikuwa na makosa na kumsahihisha.
Hii sio mara ya kwanza Rais Trump kushambuliwa mitandaoni kwani mwezi Machi mwaka huu gazeti la Washington Post lilimshambulia kwa makosa ya kimaandishi mtandaoni.