Habari

Rais Trump kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel

Rais wa Marekani Donald Trump leo anatarajia kupeleka Ofisi za Ubalozi wa Marekani  wa nchini Israel kutoka mjini Tel Aviv na kuzihamishia katika mji wa Jerusalem.

Tokeo la picha la jerusalem
Mji wa Jerusalem

Hatua hiyo itaambatana na Marekani kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel hatua ambayo imezua gumzo duniani kote kuhusu uhalali wa mmiliki wa mji huo.

Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu ya white house Sarah Sanders amesema kuwa Rais Trump alizungumza na baadhi ya viongozi jana kuhusu mipango yake ya kuhamishia ubalozi huo mjini Jerusalemu kwa manufaa ya taifa la Marekani.

Amezungumza na baadhi ya viongozi asubuhi ya jana na atendelea kuwa na majadiliano na wadau wanaohusika lakini atafanya maamuzi yenye umuhimu kwa Marekani”ameeleza Bi. Sarah kwenye mahojiano yake na kituo cha FOX.

Wakati hayo yakiendelea viongozi wa nchi za kiarabu ikiwemo Misri, Jordan na Saudi Arabia, na wenyewe Palestina wametoa onyo kwa rais Trump kuwa kuhamishia ubalozi huo Jerusalem kutadhoofisha kabisa juhudi za kuleta amani mashariki ya kati.

Mji wa Jerusalem ulikuwa hautambuliki umiliki wake kwani umekuwa ukimilikiwa na pande mbili za Palestina na Israel.

Hata hivyo, Palestina imekuwa ikiamini kuwa mji wa Jerusalem ni makao makuu yao ya baadae pindi watakapotangazwa na umoja wa mataifa kuwa taifa huru.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents