Tupo Nawe

Rais Putin afanya mazoezi ya Judo kumuonesha Trump ukakamavu wake, apigana na vijana 30 (video)

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameonesha kuwa yeye afya yake sio mgogoro licha ya kwamba umri wake ni mkubwa.

Putin mwenye miaka 66 alhamisi ya wiki hii alienda kwenye kituo cha mazoezi ya Judo mjini Sochi ambapo alionekana bado mwili wake upo FITI.

Kwenye mazoezi hayo, alifanya kwa takribani dakika 55 na alifanikiwa pia kupambana na mshindi wa Medali ya shaba kwenye michuano ya olimpiki mwaka 2016 Natalia Kuzyutina.

Mazoezi hayo yanakuja, ikiwa ni siku 5 zimepita tangu daktari wa Rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kuwa afya yake haipo sawa kwani ameongezeka uzito. Tazama mazoezi ya Rais Putin hapa chini

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW