Habari

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa kuukosa mkutano wa UN kutokana na machafuko nchini kwake

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa kuukosa mkutano wa UN kutokana na machafuko nchini kwake

Raisi wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa hatahudhuria mkutano mkuu wa umoja wa mataifa jijini New York, baadae mwezi huu. Badala yake, amesema atabaki nchini humo kushughulikia changamoto zinazokabili nchi yake kwa sasa ikiwemo vitendo vya mashambulizi ya chuki dhidi ya raia wa kigeni na unyanyasaji dhidi ya wanawake.

Nchini Afrika Kusini, miongoni mwa vichwa vya habari juma lililopita ilikuwa ni taarifa kuhusu ubakaji na mauaji ya wanawake na watoto katika sehemu kadhaa za nchi.

Iliwaacha wanawake wengi wakijiuliza: “Je! nitafuata mimi!

Kesi moja iliyemhusisha mtu mwenye hadhi kubwa, mfanyakazi wa ofisi ya posta ambaye alikiri kubaka na kumuua mwanafunzi wa miaka 19 Uyinene Mrwetyana. Ilikuwa ni wakati ambao uliwafanya wanawake kuhisi hatari na hofu.

Takwimu za hivi karibuni za uhalifu, ambazo zilitolewa Alhamisi, zilidhihirisha kwamba hofu yao ni dhahiri. Mauaji, ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia vimeongezeka.

Lakini wanawake wengi wanakataa kunyamazishwa. Siku ya Ijumaa, mamia ya wanawake, ambao walikuwa wamevaa mavazi ya rangi nyeusi, walianza kukusanyika Johannesburg saa za asubuhi ili kuongeza uelewa dhidi ya dhuluma ya kijinsia.

Wanawake wengi walikuwa wakilia. Baadhi ya waandamanaji walikua wamebeba mabango yakiwa na ujumbe wa kuomba kukomeshwa kwa vitendo hivyo.

Makosa ya unyanyasaji wa kijinsia na mauaji vimeongezeka sana nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, kulingana na takwimu mpya za uhalifu.

Wauaji waliorekodiwa na polisi wamekuwa wakiongezeka kila mwaka kwa muongo mmoja uliopita, na makosa ya unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji yameongezeka kwa asilimia 4.6 mwaka huu.

Kutolewa kwa takwimu hizo kunakuja huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu dhuluma dhidi ya wanawake baada ya visa vingi vya ubakaji na mauaji katika wiki chache zilizopita.

Maelfu ya watu waliingia barabarani mapema mwezi huu kuandamana dhidi ya vitendo hivyo.

Kati ya makosa ya udhalilishaji wa kingono, unyanyasaji wa kijinsia uliongezeka kwa 9.6% na ubakaji kwa 3.9%.

Waafrika kusini wameghadhabishwa na msururu wa visa vya ubakaji na mauaji ya wanawake katika wiki za hivi karibuni – kikiwemo cha msichana wa shule aliyevunjwa fuvu la kichwa na mwanafunzi wa chuo kikuu aliyepigwa kwa kifaa butu hadi kufariki.

Ubakaji na mauaji yamechangia maandamano na kampeni ya #AmINext campaign katika mtandao wa kijamii Twitter, na waraka uliotiwa saini na zaidi ya watu 500,000 kutaka kurudishwa kwa hukumu ya kifo katika taifa linalokabiliana na viwango vya juu vya uhalifu.

Kwa mujibu wa BBC. Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ameahidi msururu wa hatua kukabiliana na mzozo – ikiwemo kuidhinisha daftari la wahalifu, kuongeza idadi ya “mahakama maalum ya wahalifu wa unyanyasaji wa kingono”, na hukumu kali zaidi.

Mpiga picha Sarah Midgley, mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 37 anayeishi katika mji wa Johannesburg, bado anapata unafuu kutokana na athari za kubakwa tariban muongo mmoja uliopita.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents